Mfumuko wa bei wa asilimia 10,000,000 unafananaje?

Mfumuko wa bei wa asilimia 10,000,000 unafananaje?

10 October 2018 Wednesday 11:10
Mfumuko wa bei wa asilimia 10,000,000 unafananaje?

Mfumuko wa bei wa asilimia milioni 10 ukoje? Wakati kitu leo kikiwa kinauzwa shilingi 1 kinaweza kupatikana kw ash 100,000, je, ipo njia ya kukokotoa madhara yake?

Baada ya kushudia bei zikipanda kwa kiasi kisichomithilika cha asilimia 1000 mwaka jana, mfumuko wa bei mkali (hyperinflation) nchini Venezuela umelipuka Zaidi hadi kufikia asilimia milioni 1.4 mwaka huu, utabiri wa Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, uliotolewa jana unaonuejsa katika taarifa yake ya World Economic Outlook.

Lakini mwaka ujao wa 2019, mfumuko wa bei mkali unatarajiwa kufikia asilimia milioni 10, wasomaji wa taarifa hiyo walilazimika kuhesabu idadi ya sifuri kwenye hiyo namba kuhakikisha kuwa ilikuwa ni sahihi.

Ni jambo baya kwamba taifa hilo la Amerika Kusini liliachwa katika ujumuishaji wa pamoja wa mfumuko wa bei wa ukanda huo kwa kuwa ungeharibu wastani mzima.

Baada ya miaka mingi ya usimamizi mbovu wa uchumi, huku sekta muhimu zikiwa zimesimama bila kupiga hatua yoyote mbele, Venezuela imeshuhudia makumi ya maelfu ya watu wakiikimbia nchi hiyo kila siku, wakitafuta chakula na madawa, na kujazana katika mataifa ya jirani ya Colombia na Brazil.

Uchumi wa Venezuela ulisinyaa kwa asilimia 14 mwaka jana na unatarajiwa kuendelea na hali hiyo kwa asilimia 18 mwaka huu.

Kipato cha mtu mmoja mmoja kinatathminiwa kushuka kwa zaidi ya asilimia 35 kuanzia mwaka 2013-17 na kinatarajiwa kuanguka zaidi kukaribia asilimia 60 kati ya 2013-2023, IMF imesema.

Wakati habari sio mbaya sana katika maeneo mengine, IMF inapunguza ukuaji wa uchumi wa dunia hadi asilimia 3.7 mwka huu na ujao, kutokana na kupungua kwa biashara kulikosababishwa na vita ya kibiashara baina ya Marekani na China.

Updated: 27.05.2019 11:08
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.