TRA yasitisha mkataba na mawakala wa mashine za EFD

TRA yasitisha mkataba na mawakala wa mashine za EFD

18 May 2018 Friday 14:16
TRA yasitisha mkataba na mawakala wa mashine za EFD

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesitisha mkataba wa kuwatumia mawakala kugawa mashine za EFD badala yake kazi hiyo itafanywa na yenyewe.

Hayo yamebainishwa bungeni leo na naibu waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji wakati akijbu swali la msingi la Mbunge wa Nsimbo Richard Mbogo (CCM) aliyetaka kujua kama TRA inakubali ushahidi wa malipo kw anjia muamala ya simu za mkononi.

Mbunge huyo alitaka kujua endapo serikali itakuwa tayari kupokea maelezo endapo simu itapotea au kumbukumbuku kufutika.

Akijibu Naibu waziri Kijaji alisema mawakala wameiingizia mamlaka hiyo gharama zisizo na msingi na kwa sasa kazi ya kusambaza mashine hizo itafanywa na TRA yenyewe.

Kuhusu utunzaji wa kumbukumbu alisema kuwa sheria ya kodi ya mwaka 2015 inamtaka mlipa kodi kutunza kumbukumbu za kielektoniki na zile ngumu (makaratasi) ya malipo yote anayofanya kwa kipindi cha miaka mitano.

Alidokeza kuwa serikali ina mpango wa kuendelea kutoa mashine za EFD kwa wafanyabiashara wa kati kwa kuwauzia.

Alisema kuwa hata wafanyabiashara wakubwa walikuwa wanalipa kununua mashine hizo kwa kukatwa moja kwa moja baada ya kufanya mauzo, tofauti na awali kuwa eti ziilikuwa zinatolewa bure.

Kwa mujibu wa Naibu waziri Kijaji, zoezi la kutoa mashine hizo kwa wafanyabiashara wa kati linatarajia kuanza tarehe 1, Julai 2018.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.