Trump abanwa kila kona

Trump abanwa kila kona

01 June 2018 Friday 17:13
Trump abanwa kila kona

UMOJA wa Ulaya umesema kuwa umejipanga kujibu uamuzi wa serikali ya Rais wa Marekani Donald Trump juu ya hatua yake aya kuweka ushuru kwa bidhaa za pua na bati zinazoingizwa Washington.

Imeripotiwa kuwa Canada na Mexico zilitangaza mara moja hapo jana hatua za kujibu ushuru mpya uliowekwa na Marekani dhidi ya bidhaa zao za chuma cha pua na bati zinazoingizwa kwenye soko la nchi hiyo.

Waziri wa fedha wa Ujerumani Peter Altmeier amezungumzia uwezekani wa kushirikiana na Canada pamoja na Mexico, kuratibu mkakati wa pamoja dhidi ya Marekani.

Tangazo hapo jana kutoka kwa waziri wa biashara wa Marekani Wilbur Ross la kuanzisha rasmi vikwazo vya kiushuru dhidi ya Umoja wa Ulaya, Canada na Mexico lilihitimisha kipindi cha miezi kadhaa ya sintofahamu, juu ya iwapo Marekani ingeelea kuziondoa nchi hizo kwenye orodha yake ya vikwazo vya kibiashara.

Katika hatua hizo, bidhaa zote za chuma cha pua zinazoingizwa Marekani kutoka Umoja wa Ulaya, Canada na Mexico ushuru wake umeongezwa kawa asilimia 25, na ongezeko la asilimia 10 limewekwa dhidi ya bidhaa za bati.

Akizungumza mjini Brussels muda mfupi baada ya uamuzi wa Marekani, Rais wa kamisheni ya Ulaya Jean Claude Juncker alionekana dhahiri kuchukizwa, aliulaani uamuzi huo.

Rais wa Kamisheni ya Ulaya Jean Claude Juncker amesema Ulaya haitajikunyata mbele ya vikwazo vya Marekani

''Hii ni siku mbaya kwa biashara ya dunia. Ulaya haiwezi kukaa kimya kuhusiana na hatua kama hizi. Tutafikisha mara moja malalamiko katika Shirika la Kimataifa la Biashara, na mnamo saa chache zijazo, tutaweka wazi mpango wetu wa kulipiza kisasi.'' Amesema Juncker na kuongeza kuwa inachoweza kukifanya Marekani dhidi ya Ulaya, Ulaya pia inaweza kukifanya dhidi ya Washington.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.