Wizara Madini, Fedha kukusanya bilioni 475

Wizara Madini, Fedha kukusanya bilioni 475

17 June 2019 Monday 14:48
Wizara Madini, Fedha kukusanya bilioni 475

Na mwandishi wetu, Dodoma
WIZARA ya Madini na wizara ya Fedha na Mipango zimesaini makubaliano ya kimkakati ya ukusanyaji wa maduhuli kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ya bilioni 475.

Hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo imefanyika leo Juni 17, 2019 jijini Dodoma, na kuhudhuriwa na viongozi waandamizi wa wizara hizo.

Akizungumza kabla ya kusaini makubaliano hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Doto James amesema  wizara yake itatoa kiasi cha bilioni 10.7 kama fedha zitakazotumika kwenye mradi wa kimkakati wa ukusanyaji wa maduhuli kulingana na vigezo vilivyotolewa.

"Lengo la kutoa fedha hizi ni kuiwezesha Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini kufikia lengo la ukusanyaji wa maduhuli lililowekwa kwa mwaka wa fedha 2019/2020 la shilingi bilioni 475,'' amesema.

Katibu mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kwa kutoa kiasi hicho cha fedha.
 
Amesema fedha hizo zitatumika kununulia  vifaa vya kupimia madini pamoja na magari yatakayotumika kufika sehemu zote zenye shughuli za uchimbaji wa madini na kukusanya maduhuli.

Katika hatua nyingine, Profesa Msanjila amesema mchakato wa kuwapata watumishi wapya wa tume ya madini unaendelea vizuri. 

Naye Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema wanaendelea kusimamia kwa karibu zaidi masoko ya madini yaliyoanzishwa hivi karibuni nchini kote.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.