Aishi na maiti ya mama yake kwa miaka mitatu

Aishi na maiti ya mama yake kwa miaka mitatu

12 July 2019 Friday 14:40
Aishi na maiti ya mama yake kwa miaka mitatu

Texas, Marekani
MWANAMKE mmoja jimboni Texas, nchini Marekani amekamatwa baada ya mabaki ya maiti ya mama yake inayooza kugunduliwa nyumbani anakoishi.

Polisi wanaamini mwanamke huyo(mama) mwenye umri wa miaka 71 alianguka  na kupata majeraha mnamo mwaka 2016.

Wanatuhumu kwamba binti yake mwenye umri wa miaka 47 alishindwa kumhudumia vizuri mama yake aliyefariki "siku chache baadaye" kutokana na athari ya kuanguka huko.

Mabaki ya mwili wa marehemu yalipatikana kwenye sakafu ya chumba kimoja. Binti yake na mjukuu wake marehemu walilala katika chumba cha pili katika nyumba hiyo.

Mjukuu wa marehemu alikuwa na miaka 15 wakati akiishi na maiti ya bibi yake. Na kutokana na hilo, mama yake ameshtakiwa kwa 'kumdhuru mtoto' wa chini ya miaka 15.

Mjukuu huyo sasa anatazamwa na jamaa zao na anapokea usaidizi kutoka kitengo cha kuwalinda watoto.

Huenda mama yke akakabiliwa na hadi miaka kifungo cha miaka 20 gerezani na faini ya hadi  dola 10,000.

Polisi wanasema marehemu bibi huyo aliheshimika katika jamii kwenye eneo hilo, na alifanya kazi kama karani na mwalimu msaidizi katika mojawapo wa shule katika eneo hilo kwa miaka 35.

Alipostaafu, alikuwa akifanya kazi ya kukusanya tiketi katika sherehe za michezo huko Seguin.

BBC

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.