Mtoto wa rais alaani kauli ya baba yake dhidi ya Watanzania

Alikuwa akiuelezea ujumbe wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ambao ulikuwa ukiipinga Marekani katika kura dhidi ya kuitambua China na kuiondoa Tawain katika UN

Mtoto wa rais alaani kauli ya baba yake dhidi ya Watanzania

Alikuwa akiuelezea ujumbe wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ambao ulikuwa ukiipinga Marekani katika kura dhidi ya kuitambua China na kuiondoa Tawain katika UN

03 August 2019 Saturday 08:03
Mtoto wa rais alaani kauli ya baba yake dhidi ya Watanzania

Washington, Marekani
MTOTO wa kike wa rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan, Patti Davis amesema 'hakuna la kujitete' kwa kauli aliyotoa baba yake  mwaka 1971 katika mazungumzo ya simu.

Kanda mpya ya sauti umefichua Reagan -ambaye wakati huo alikuwa Gavana wa California - aliuelezea ujumbe wa Afrika katika Umoja wa Mataifa kama "tumbili". Patti Davis amelaani vikali katika waraka wake uliochapishwa katika gazeti la Washington Post.

"Hakuna la kujitetea, hakuna ufafanuzi wa maelezo, hakuna ufafanuzi mzuri juu ya kile ambacho baba yangu alikisema," aliandika.

Bi Davis aliandika katika waraka kwa ajili ya gazeti la Washington Post kwamba alikuwa anajianda kumtetea baba yake kabla ya kusikia kanda ya sauti, lakini alishituka baada ya kusikia kile alichokisema rais huyo wa zamani.

"Siwezi kuwaambia kuhusu mwanaume aliyekuwa akiongea kwa simu ," aliandika . "si mwanaume niliyemfahamu mimi."

Alichokisema Ronald Reagan kwa watanzania!
Sauti iliyorekodiwa hivi karibuni ilionekana kwa mara ya kwanza katika gazeti la The Atlantic.

Reagan alitoa kauli katika mazungumzo na rais wa Marekani aliyekuwa madarakani wakati huo, Richard Nixon. Alikuwa akiuelezea ujumbe wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa(UN), ambao ulikuwa ukiipinga  Marekani katika kura dhidi ya kuitambua China na kuiondoa Taiwan katika Umoja wa Mataifa.

Reagan alimpigia simu rais siku iliyofuata ,akimwambia : "Aangalie hao ... tumbili kutoka hizo nchi Afrika - ambao bado hawafurahii kuvaa viatu!"

Nixon anasikika kwenye kanda hiyo akiangua kicheko kwa sauti kubwa baada ya kauli hiyo.
Patti Davis alisema kanda ilimshitua . "ninataka kurejea nyuma wakati bado sijasikia sauti ya baba yangu akisema maneno."

Aliandika maneno aliyoyasikia "Yatabaki nami daima ", na akasema kama baba yake angekuwa bado hai "angeomba msamaha " kama angesikia sauti yake iliyorekodiwa.

Kauli zake "Haziwezi kueleweka kwa maneno mengine isipokuwa ubaya ", Bi Davis aliandika. Aliongeza kuwa anatumai watu watamsamehe rais huyo wa zamani wa marekani "kwa maneno ambayo hayangepaswa kutamkwa katika mazungumzo yoyote yale ," na ambayo "kwetu tuliomfahamu Ronald Reagan, yatabakia kuwa si ya kawaida."

Wakosoaji wanamshutumu Reagan kuwa mbaguzi wa rangi katika kipindi chake chote cha maisha ya kazi.

Alipokuwa akigombea kiti cha ugavana wa California mnamo mwaka 1966, mchezaji huyo wa zamani wa filamu alisema "kama mtu binafsi anataka kuwabagua waniga (Negroes) au wengine katika kuuza au kukodisha nyumba, ni haki yake kufanya hivyo ".

BBC

Updated: 03.08.2019 08:21
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.