Mtoto wa rais Trump atemewa mate

Mtoto wa rais Trump atemewa mate

27 June 2019 Thursday 06:33
Mtoto wa rais Trump atemewa mate


Eric Trump, mtoto wa kiume wa rais wa Marekani Donald Trump, amesema kuwa alitemewa mate katika baa moja ya kifahari mjini Chicago .

''Kilikuwa kitendo cha kuchukiza na mtu ambaye ana matatizo ya kihisia''  Eric Trump aliuambia mtandao wa Breitbart .

Mfanyakazi huyo alihojiwa na majasusi na baadaye kuachiliwa , kulingana na chombo kimoja cha habari.
Baa hiyo ilithibitisha kwamba kisa kisichokuwa cha kawaida kilimkumba mwana huyo wa Trump.

''Hatukushuhudia kisa hicho na ndio tunaanza kujua kilichotokea'', taarifa ya baa hiyo inaeleza.

''Kile kinachojulikana ni kwamba hakuna mteja anayefaa kutemewa mate''.
Bwana Trump aliambia mtandao wa Breitbart kwamba alikataa kuwasilisha malalamishi dhidi ya mfanyakazi huyo ambaye amepewa likizo ya lazima na baa hiyo.

Msemaji wa idara ya polisi ya mjini Chicago amethibitisha katika mtandao wa Twitter kwamba maafisa waliwasaidia majasusi hao siku ya Jumanne jioni.

Kisa hicho kilitokea katika baa ya Aviary, mgahawa maarufu ulioshinda tuzo la James Beard katika jimbo la Chicago eneo la West Loop.
Kulingana na chombo kimoja cha habari katika eneo hilo , bwana Trump alikuwa katika baa hiyo mwendo wa 01:30 GMT siku ya Jumanne wakati alipotemewa mate na mfanyakazi.

Mmiliki mwenza wa baa hiyo Nick Kokonas , aligonga vichwa vya habari mnamo mwezi Januari mwaka huu wakati alipoialika timu ya Clemson Tigers, mabingwa wa ligi ya soka nchini humo chakula cha jioni kusherehekea katika mgawaha wake wa Alinea baada ya rais kuwaalika na kuwapatia wachezaji hao chakula cha haraka katika Ikulu ya Whitehouse.

Rais Trump ambaye alikuwa mwenyeji wa timu hiyo alitoa fedha zake binafsi kulipia maankuli hayo.

Bwana Trump ambaye ni naibu wa rais wa shirika la Trump alikuwa mjini Chicago kutembelea hoteli ya Trump.
Aliambia mtandao wa Breitbart kwamba anaamini tukio hilo lilishinikizwa kisiasa.

''Kwa chama kinachoeneza injili ya uvumilivu hiki chama cha Democrats hakina tabia nzuri,'' alisema mwana huyo wa tatu wa rais Trump akidai kwamba mfanyakazi huyo alikuwa mwanachama wa Democrat.

''Hatua hiyo inasisitiza kuwa wamekata tamaa kutokana na ukweli kwamba tutaibuka washindi''.
Madai hayo ya kutemewa mate ni miongoni mwa msururu wa visa ambapo mtu wa familia ya rais Trump amenyanyaswa ama hata kukaripiwa kutokana na sera tofauti wakati anapokula.

Mnamo mwezi Juni mwaka jana ,wanarahakati walimzoma katibu wa kampuni ya Homeland Security Kristjen Nielsen katika mgahawa mmoja mjini Washington DC .

Siku chache baadaye aliyekuwa katibu wa maswala ya vyombo vya habari Sarah Sanders alitakiwa kuondoka katika mgahawa wa Lexington , Virginia kwa kuwa alikuwa akiufanyia kazi utawala wa rais Trump.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.