Neno kuthibitisha laondolewa kwenye taarifa ya pamoja ya Trump , Kim

Trump na Kim walitia saini nchini Singapore taarifa ya pamoja ambapo serikali ya mjini Pyongyang iliahidi kufanya kazi kuelekea hatua ya kuondoa kabisa...

Neno kuthibitisha laondolewa kwenye taarifa ya pamoja ya Trump , Kim

Trump na Kim walitia saini nchini Singapore taarifa ya pamoja ambapo serikali ya mjini Pyongyang iliahidi kufanya kazi kuelekea hatua ya kuondoa kabisa...

13 June 2018 Wednesday 10:00
Neno kuthibitisha laondolewa kwenye taarifa ya pamoja ya Trump , Kim

Na Mwandishi Wetu

KATIBU mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameukaribisha mkutano wa kilele uliofanyika kati ya rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong UN akisema ni hatua muhimu ya msingi kuelekea hatua ya kuondolewa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea.

Guterres amewatolea mwito wahusika wote kuitumia fursa hii na kusema Umoja wa Mataifa utasaidia katika kufikia lengo la kuukongoa mradi wa silaha za nyuklia za Korea Kaskazini.

Trump na Kim walitia saini nchini Singapore taarifa ya pamoja ambapo serikali ya mjini Pyongyang iliahidi kufanya kazi kuelekea hatua ya kuondoa kabisa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea lakini neno kuthibitisha halikuonekana katika taarifa hiyo.

Kutumiwa neno kuthibitisha ingemaanisha kwamba nchi hiyo inakubali ukaguzi ya kimataifa katika vituo vyake vya kijeshi ili kuthibitishwa kwamba silaha za Nyuklia na miradi ya kuzitengeneza imekongolewa.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.