banner68
banner58

Trump, Kim waandika historia ya kwanza ya dunia

Kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo ya kihistoria Trump alionekana mwenye matumaini. Kupitia mtandao wake wa Twitter amesema mkutano huo, wa kwanza kabisa...

Trump, Kim waandika historia ya kwanza ya dunia

Kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo ya kihistoria Trump alionekana mwenye matumaini. Kupitia mtandao wake wa Twitter amesema mkutano huo, wa kwanza kabisa...

12 June 2018 Tuesday 09:28
Trump, Kim waandika historia ya kwanza ya dunia

Na Mwandishi Wetu

HATIMAYE historia imetumia mara baada ya mahasimu wa miaka mingi, yaani Korea ya Kaskazni na Marekani kukuktana na kujadiliana kwa faragha kuhusu nyuklia.

Taarifa zinaonyesha kuwa mkutano baina ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong –un na Rais wa Marekani Donald Trump, umefanyika leo mapema huko Singapore

Trump na Kim wamepigwa picha wakishikana mikono kabla ya kuanza mazungumzo ya faragha.

Trump alikuwa wa kwanza kuwasili kwenye hotel hiyo saa mbili na dakika chache muda wa Singapore, akifuatiwa na Kim, aliyeingia na msafara wa magari yapatayo 20.

Kulingana na ratiba ya mazungumzo hayo, Trump na Kim wamekutana peke yao kwenye meza ya mazungumzo, wakisindikizwa tu na wakalimani wao. Baadaye ilitarajiwa kwamba maafisa wa pande zote wangejiunga na mkutano huo, katika mazungumzo ambayo yataendelea hadi wakati wa chakula cha mchana. Inatarajiwa kwamba baada ya mazungumzo hayo Rais Trump atazungumza na waandishi wa habari, na kisha kupanda ndege na kuondoka kurudi mjini Washington.

Kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo ya kihistoria Trump alionekana mwenye matumaini. Kupitia mtandao wake wa Twitter amesema mkutano huo, wa kwanza kabisa kati ya kiongozi wa Korea Kaskazini na Rais wa Marekani aliyeko madarakani, ungekuwa na matokeo ya kufurahisha kwa Korea Kaskazini na kwa dunia nzima.

Lakini pia hakukosa vijembe kwa wakosoaji wake, ''Wenye chuki na walioshindwa wanasema hali ya kwamba nimekuja katika mkutano huu ni hasara kwa Marekani'', alidhihaki Trump kupitia ukurasa wake wa twitter.

Aliendeleza mashambulizi akisema wachambuzi hawana kingine cha kusema, licha ya kwamba amefanikiwa kuwakomboa raia wa Marekani waliokuwa wakishikiliwa nchinin Korea Kaskazini.

Hakuna mengi yanayojulikana kuhusu mazungumzo hayo hadi pale taarifa itakapotolewa baadaye, lakini waziri wa mabo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo, akizungumza jana mjini Singapore amesema Marekani haitaridhishwa na chochote mbali na kuondolewa kikamilifu kwa silaha za nyuklia kwenye rasi ya Korea, ambako kunathibitishwa na ukaguzi, kwamba ni hatua isiyoweza kurudi nyuma.

Azania Post

Updated: 12.06.2018 09:52
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.