banner68
banner58

Trump, Kim watafuna mabilioni ya shilingi kwa siku moja huko Singapore

Trump na Kim wamekutana mapema leo huko Singapore katika mkutano wa siku moja tu ambao umehudhuriwa na wakalimani wao tu

Trump, Kim watafuna mabilioni ya shilingi kwa siku moja huko Singapore

Trump na Kim wamekutana mapema leo huko Singapore katika mkutano wa siku moja tu ambao umehudhuriwa na wakalimani wao tu

12 June 2018 Tuesday 09:52
Trump, Kim watafuna mabilioni ya shilingi kwa siku moja huko Singapore

Na Mwandishi Wetu

GHARAMA za maandalizi ya mkutano kati ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un na Rais wa Marekani Donald Trump inakisiwa kuwa zimefikia dola milioni 20 ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi bilioni 45 za kitanzania.

Akizungumza, Waziri Mkuu wa Singapore Lee Hsien Loong alisema kuwa wamelazimika kutumika gharama hizo kwa ajili ya kusaidia juhudui za kimataifa za kuleta amani duniani.

Trump na Kim wamekutana mapema leo huko Singapore katika mkutano wa siku moja tu ambao umehudhuriwa na wakalimani wao tu.

Alisema kuwa asilimia kubwa ya fedha hizo zimetumika kwa ajili ya masuala ya ulinzi kutokana na asili ya mkutano wenyewe na kile kinachojadiliwa baina ya viongozi hao.Akifafanua alisema kuwa kuna maelfu ya wanausalama wamekuwa wakilinda eneo la mkutano kuanzia anga, baharini na nchi kavu.

“Hii ni operesheni kubwa sana kwa sababu ni mkutano wa kimataifa ambao kamwe hatuwezi kufanya makosa ya aina yoyote” , alisema

Aliongeza kuwa Singapore inaweza kufanya mkutano huo ufanyike bila kuhesabu kila gharama lakini lengo ni kufakinisha maazimio.

Azania Post

Updated: 12.06.2018 16:21
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.